Daily Archives: November 4, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Spika wa Bunge la China, Beijing nchini China

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Li Zhanshu, Beijing nchini China.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na ujumbe aliombatana nao kwenye mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Li Zhanshu Beijing nchini China.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Modest Jonathan Mero (Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Michezo ya Kubahatisha (GBT).

Balozi Mero ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya African Discovery Group, New York nchini Marekani.

Uteuzi huu unaanza mara moja.