Monthly Archives: December 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AFUNGA NJIA YA KUCHEPUSHA MAJI NA KUANZA UJAZAJI WA MAJI BWAWA LA JNHPP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameshuhudia shughuli ya kufunga njia, kuchepusha maji na kuanza ujazaji maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Mradi huu ulianza mwaka 2018 baada ya Serikali ya Tanzania kupata Kandarasi ya ujenzi ubia wa kampuni ya Arab Contractors na El-Sewedy kutoka Misri.

Rais Samia amesema mradi huu ni mojawapo ya miradi mikubwa ya umeme barani Afrika ambapo bwawa hilo litaweza kuweka akiba kubwa ya maji na kuzalisha umeme hata mvua inapopungua.

Pia Rais Samia amesema mbali na kusaidia kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara ya mto Rufiji bwawa hili litawezesha kilimo cha uhakika cha umwagiliaji.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameagiza Wakuu wa Mikoa kuwazuia wananchi wanaochepusha maji katika maeneo mbalimbali hasa katika Bonde la Mto Rufiji na kurejesha maji katika mikondo yake ya asili kwa kuzingatia kanuni za mgawanyo wa maji.

Vile vile Rais Samia amezitaka Wizara husika kutokutoa vibali vya matumizi ya maji na uwekezaji kwenye shughuli za uzalishaji unaohitaji maji mengi katika maeneo ya juu ya bonde (upstream) na badala yake utumike uwanda wa chini wa mradi.

Kukamilika kwa Mradi wa JNHPP ambao umefikia asilimia 78.68 kutaimarisha na kufungua fursa nyingi za utalii katika eneo la kusini mwa Tanzania hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na hivyo kutoa ajira kwa wananchi.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan awaapisha Makatibu Wakuu Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 21 Desemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kaspar Mmuya kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Hashil Twaib Abdallah kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kaspar Mmuya akila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Twaib, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kaspar Mmuya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Twaib, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022. Wengine katika picha ni, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Kattanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Makatibu Wakuu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.