UTEUZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-
- Amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Bw. Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.
- Aidha, amemteua Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).
Dkt. Mwamba anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.