Daily Archives: January 16, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

  • Amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).  Prof. Ame anachukua nafasi ya Mhandisi John S. Nduguru. Prof. Ame ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  • Amemteua Bw. Eliud Betri Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Airtel Tanzania.  Bw. Sanga anachukua  nafasi ya Gabriel Malata aliyeteuliwa kuwa Jaji. 

Bw. Sanga ni Mkurugenzi wa zamani wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

  • Amemteua Jaji (Mstaafu) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti na Bw. Mohamed Khamis Hamadi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kipindi cha pili.

Aidha, Rais Samia amewateua Makamishna wa Tume kama ifuatavyo:-

  • Bw. Thomas Paulo Masanja, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.
  • Bi. Amina Talib Ali, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.
  • Bw. Khatibu Mwinyi Khatibu, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.
  • Bw. Nyanda Josiah Shughuli, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Utuezi huu ni kuanzia tarehe 15 Januari, 2023.