Daily Archives: February 9, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Mhandisi Musa Ally Nyamsingwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

Mhandisi Nyamsingwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Barabara Kuu na Usafirishaji, Kampuni ya NORPLAN Tanzania Limited.

Uteuzi huu umeanza tarehe 07 Februari, 2023.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Ephraim Balozi Mafuru kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mafuru alikuwa Mkuu wa Masuala ya Biashara katika kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Morogoro.

Uteuzi huu umeanza tarehe 08 Februari, 2023.