Daily Archives: February 14, 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ashuhudia utiaji Saini Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9. Hafla ya utiaji saini Mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Maharage Chande akiwa pamoja na Mwanasheria wa Shirika hilo Zaharani Kisilwa wakati wakitia saini Mikataba mbalimbali ya Gridi Imara na Wakandarasi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
.
.
.
.
.
.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini REA Eng. Hassan Saidy pamoja na Mwanasheria wa REA Mussa Muze wakati wakitia saini Mikataba ya kupeleka Umeme maeneo mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

  1. Amemteua Bw. Antony Diallo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA). Bw. Diallo anachukua nafasi ya Prof. Anthony Mshandete ambaye amemaliza muda wake. 

Uteuzi huu umeanza tarehe 09 Februari, 2023.

  1. Amemteua Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Marwa Waitara kwa kipindi kingine kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA). 

Uteuzi huu umeanza tarehe 13 Februari, 2023.