Daily Archives: February 27, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Said Ally Mohamed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania. 
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Mohamed alikuwa ni Mkurugenzi wa Huduma za Ufundishaji, Mafunzo na Mitihani, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT). 
Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2023.