Monthly Archives: March 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.
Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023. Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuonesha Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris nakshi za michoro ya milango ya Zanzibar pamoja na madirisha yake katika ukumbi wa Kikwete mara baada ya mazungumzo yao , Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI YA TAKUKURU NA CAG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi na watendaji wa Serikali kuzisoma na kuzielewa vyema taarifa za rushwa na za ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ziwasaidie kujitathmini.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo mara baada ya kupokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika hafla iliyofanyika Ikulu.

Aidha, Rais Samia amesema taarifa hizo hizo zinasaidia kusimamia na kuimarisha utawala bora na kuhakikisha udhibiti na usimamizi wa rasilimali za Serikali unafanywa kikamilifu.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameitaka Mamlaka ya Bandari kufanya kazi na sekta binafsi ili kuimarisha mifumo ya TEHAMA ya ukusanyaji fedha ambapo itasaidia kudhibiti upotevu mkubwa wa fedha unaotokea bandarini.

Rais Samia pia amegiza kufanyiwa tathmini kwa Mashirika ya Umma yaliyopata hasara na kuyafuta Mashirika ambayo hayana tija kwa taifa kwa kuwa Mashirika hayo yanatumia gharama kubwa lakini hayaleti faida kwa Serikali.

Katika ripoti ya CAG jumla ya Halmashauri 14 nchini zimepata hati zenye mashaka zikiwemo Halmashauri ya Jiji la Arusha, Babati, Bahi, Geita, Kilindi, Mbinga, Musoma, Nkasi, Nyasa, Simanjiro, Songwe, Sumbawanga Manispaa pamoja na Ushetu iliyopata hati mbaya.