Daily Archives: March 16, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Makatibu Tawala wa Mikoa watatu (3) na kuwahamisha vituo vya kazi wengine watatu (3).  Aidha, Mhe. Rais amefanya uteuzi wa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.  Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

A: Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa:

  1. Bw. Ally Senga Gugu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.  Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gugu alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
  •  Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.  Bw. Nzunda anachukua nafasi ya Bw. Willy Machumu ambaye amestaafu.
  • Bw. Gerald Msabila Kusaya, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.  Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kusaya alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.
  • Bw. Aretas James Lyimo kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.  Bw. Lyimo anachukua nafasi ya Bw. Gerald Kusaya ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

B: Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo:

Mhe. Rais Samia amewahamisha vituo vya kazi Makatibu Tawala wa Mikoa wafuatao:-

  1. Dkt. Fatuma Ramadhani Mganga, amehamishwa kutoka Mkoa wa Dodoma kwenda Mkoa wa Singida.  Dkt. Mganga anachukua nafasi ya Bi. Dorothy Aidan Mwaluko ambaye amestaafu.
  • Bw. Rashid Kassim Mchata, amehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda Mkoa wa Pwani.  Bw. Mchata anachukua nafasi ya Bi. Zuwena Omari Jiri ambaye amehamishiwa Mkoa wa Lindi.
  • Bi. Zuwena Omari Jiri amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda Mkoa wa Lindi.  Bi. Zuwena anachukua nafasi ya Bw. Ngussa Dismas Samike ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Viongozi wote walioteuliwa katika nafasi mpya watajulishwa tarehe ya kuapishwa.