Daily Archives: March 20, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMEKUSUDIA KULETA MAGEUZI                       YA KILIMO – SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wadau wa kilimo kushirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na wataalam wa kilimo kubuni mipango ya maendeleo  itakayoleta mageuzi katika sekta hii.

Rais Samia ametoa wito huo leo kwenye uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja (block farming); utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji; na kukabidhi mitambo na magari kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji iliyofanyika Chinangali, wilayani Chamwino.

Aidha, Rais Samia amesema uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja ni mwendelezo wa jitihada za Serikali katika kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa vijana na wanawake kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyo bora (Building a Better Tomorrow – BBT).

Vile vile, Rais Samia amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imejidhatiti kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu na unafikia mafanikio yaliyokusudiwa.

Rais Samia Pia amesema miongoni mwa malengo ya Serikali kwa upande wa kilimo cha mazao, uvuvi na ufugaji ni kuwa na mchango wa 10% katika pato la taifa mwaka 2030 kutoka 3.6% ya hivi sasa.

Halikadhalika, Rais Samia amemtaka Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kuhakikisha anasimamia kikamilifu fedha zote zinazotolewa katika mradi huo ili iweze kuzalisha bila kufanyiwa ubadhirifu.

Utekelezaji wa Mpango wa Mashamba Makubwa ya Pamoja kupitia BBT umeanzia mkoa wa Dodoma katika Shamba la Chinangali II lenye ekari 400.  Hekta zaidi ya 47,000 zimeshapatikana katika mikoa mingine na upimaji udongo unaendelea ili kutambua mahitaji ya virutubisho.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Mtendaji Mkuu na Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Briston, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Machi, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Briston, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani (USD) 30,000,000.00 kutoka kwa Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Briston kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Elimu, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Machi, 2023. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa Mabweni 273 pamoja na Madarasa zaidi ya 1094 kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Briston mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Briston pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Machi, 2023.