Daily Archives: March 28, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Ili kutekeleza azma hiyo amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati. Aidha, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati:

  1. Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;
  • Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;
  • Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;
  • Balozi Tuvako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa 08:30 mchana.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Ujumbe wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) pamoja na Uongozi wa Juu wa Benki ya ABSA Group ambao ni Wawekezaji wa Benki ya (NBC) Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 27 Machi, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa ABSA Group Bw. Arrie Rautenbach ambao ni Wawekezaji wenza na Serikali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Benki ya Taifa ya Biashara Tanzania (NBC) pamoja na Uongozi wa Juu wa Benki ya ABSA Group ambao ni Wawekezaji wenza na Serikali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa ABSA Group Bw. Arrie Rautenbach ambao ni Wawekezaji wenza na Serikali, mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Benki ya Taifa ya Biashara Tanzania (NBC) pamoja na Uongozi wa Juu wa Benki ya ABSA Group ambao ni Wawekezaji wenza na Serikali, mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi 2023