Daily Archives: April 3, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya vituo kwa Mabalozi wawili (02) na uteuzi wa Balozi mmoja (01) kama ifuatavyo: 

  1. Amempangia Balozi Humphrey Herson Polepole kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba.  Kabla ya uteuzi huu Balozi Polepole alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Malawi.
  •  Amemteua Balozi Lt. Jenerali (mstaafu) Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE).  Kabla ya uteuzi huu, Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Uteuzi na kupangiwa Kituo

  • Amemteua Bw. Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia Ubalozi nchini Uturuki.¬†Kabla ya uteuzi huu, Bw. Bakari alikuwa Konseli Mkuu, Dubai.

Tarehe ya uapisho wa Balozi Bakari itatangazwa baadae. 

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan awaapisha Viongozi Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 02 Aprili, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) tarehe 02 Aprili, 2023.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Simbachawene wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Simbachawene, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.