Daily Archives: April 21, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

  1. Amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President – Legal Affairs).  Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.  Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Aprili, 2023; na
  • Dkt. Richard Stanslaus Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (Advisor to the President – Climate Change and Environment).  Kabla ya uteuzi huu Dkt. Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).  Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Aprili, 2023.