Daily Archives: April 27, 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera. Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Rais kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alikuwa na shauku kubwa ya kumuona Mhe. Rais Samia. Pichani mtoto huyo akiwa haamini macho yake mara baada ya kugundua kuwa aliyekuwa anazungumza naye ni Mhe. Rais Samia, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaka wa mtoto  huyo Saddam Mustapha Baranyikwa.