Monthly Archives: May 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili Abuja nchini Nigeria kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe. Bola Tinubu Tarehe 28 Mei, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja nchini Nigeria tarehe 28 Mei 2023, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa Rais Mteule wa Nchi hiyo Mhe. Bola Tinubu, aliyeshinda kiti hicho kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Februari 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la Maua kutoka kwa Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Nigeria mara baada ya kuwasili  kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja nchini Nigeria tarehe 28 Mei 2023, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa Rais Mteule wa Nchi hiyo Mhe. Bola Tinubu, aliyeshinda kiti hicho kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Februari 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Heshima kutoka kwa Jeshi la Jamhuri ya Nigeria mara baada ya kuwasili  kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja nchini Nigeria tarehe 28 Mei 2023, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa Rais Mteule wa Nchi hiyo Mhe. Bola Tinubu, aliyeshinda kiti hicho kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Februari 2023.
.
.
.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AFUNGA MAFUNZO YA TRAMPA NA TAPSEA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kukifanya Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora kiweze kutumika kuwanoa Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kwenye ngazi ya Shahada.

Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kufunga mafunzo ya pamoja ya Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika viwanja vya Fumba.

Aidha, Rais Samia amesema lengo la kupandisha hadhi Chuo hicho ni kuandaa watendaji wenye weledi na viwango vya juu kwa kutumia mitaala mipya.

Rais Samia pia amewasisitiza Watunza Kumbukumbu na Nyaraka na Makatibu Mahsusi kufanya kazi kwa nidhamu, uadilifu na kuzingatia misingi ya utunzaji siri, miongozo na kuheshimu mipaka ya kiutendaji.

Vile vile, Rais Samia amewahimiza kufanya kazi kwa weledi katika taaluma zao na kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewaelekeza Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuzungumza na waajiri katika sekta binafsi ili kuwaruhusu na kuwasaidia wanataaluma kushiriki mafunzo hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mkutano huo kuwaleta pamoja Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kwa ajili ya kupata mafunzo maalum yenye kuwaongezea tija na ufanisi.