Daily Archives: May 9, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

  1. Amemteua Prof. Elifas Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Prof. Bisanda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kipindi cha pili.
  • Amemteua Mhandisi Abdallah Mohamed Mkufunzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maji.

Uteuzi wa Wenyeviti hao umeanza tarehe 05 Mei, 2023.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi Namibia ‘Diaspora’ tarehe 09 Mei, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Namibia (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano wa Kimtaifa wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi Maalum kutoka kwa Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.