Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Mussa Mohamed Makame, Mkurugenzi Mtendaji, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri na Uwekezaji wa Mfuko wa Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board). Aidha, Mheshimiwa Rais amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-:
- Dkt. Suleiman Magema Missango – Mkurugenzi, Kurugenzi ya Utafiti na Sera, Benki Kuu ya Tanzania (BoT);
- Bw. Safiel Fahamuel Msovu – Afisa Fedha Mwandamizi, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC);
- Bw. Shogholo Charles Msangi – Mkurugenzi wa Kampuni ya Express Microfinance Company Ltd; na
- Bi. Mwanaidi Athuman Mtanda – alikuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali.
Uteuzi huu umeanza tarehe 11 Mei, 2023.