Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:
- Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
- Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
- Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
- Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.