Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, uteuzi wa Mkuu wa Mkoa, uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na uteuzi wa Mkuu wa Wilaya kama ifuatavyo:
- Amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Mhe. Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee. Meja Jenerali Mzee atapangiwa majukumu mengine.
- Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Mhe. Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anachukua nafasi ya Mhe. Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.
- Mhe. Charles Makongoro Nyerere amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Mhe. Nyerere ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mhe. Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Manyara.
- Amemteua Bw. Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo. Anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huu unaanza mara moja.
Uapisho wa Mkuu wa Mkoa mpya utafanyika tarehe 24 Mei, 2023 saa 10:00 jioni, Ikulu Chamwino.