Monthly Archives: June 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Jaji Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha pili.
  • Amemteua Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mhe. Balozi Mapuri ameteuliwa kuwa Mjumbe kwa kipindi cha pili.
  • Amemteua Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaanza tarehe 01 Julai, 2023.

  • Amemteua Prof. Idrissa Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA). Prof. Mshoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi cha pili.
  • Amemteua Bw. Benjamin Mashauri Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi Bw. Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 25 Juni, 2023.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa AfDB anayeshughulikia Masuala ya Kilimo na Maendeleo ya Kijamii Beth Dunford Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Tarehe 28 Juni, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)anayeshughulikia Masuala ya Kilimo na Maendeleo ya Kijamii Beth Dunford aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Juni, 2023.
 
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia Masuala ya Kilimo na Maendeleo ya Kijamii Beth Dunford pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia Masuala ya Kilimo na Maendeleo ya Kijamii Beth Dunford, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Juni, 2023.