Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Agnes Richard Kayola kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi.
Balozi Kayola ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Uteuzi huu unaanza mara moja.