Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Julai, 2023 amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:
- Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
- Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama. Amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.
- Amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini.