Daily Archives: July 5, 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan atembelea Halmashauri ya Jiji la Lilongwe nchini Malawi tarehe 05 Julai, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Lilongwe Mhe. Richard Banda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Civic zilizopo katika Halmashauri hiyo nchini Malawi tarehe 05 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ufunguo kama ishara ya ukaribisho katika Jiji la Lilongwe kutoka kwa Meya wa Halmashauri ya Jiji hilo Mhe. Richard Banda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo za Civic nchini Malawi tarehe 05 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha Hati aliyokabidhiwa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Lilongwe Mhe. Richard Banda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo za Civic nchini Malawi tarehe 05 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Lilongwe nchini Malawi tarehe 05 Julai, 2023. Kulia ni Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera akiwa pamoja na Meya wa Jiji hilo Mhe. Richard Banda kushoto akishuhudia.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:

  1. Ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ambapo amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Mhe. Prof. Mkumbo ni mbunge wa jimbo la Ubungo.
  • Ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Fedha. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
  • Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
  • Amemteua Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).
  • Amemteua Bw. Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mwandumbya alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.