Daily Archives: July 15, 2023

Mhe. Rais Samia awatembelea na kuwajulia hali Viongozi mbalimbali Wastaafu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mzee Yusuf Makamba mara baada ya kuwasili Nyumbani kwake Wazo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumjulia hali tarehe 14 Julai, 2023.
 
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Mswala kutoka Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mzee Yusuf Makamba mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Wazo Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai, 2023.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakati alipokwenda nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali tarehe 14 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na kumfariji Mama Dorcas Membe Mjane wa Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Hayati Bernard Membe wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai, 2023.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Mama Dorcas Membe Mjane wa Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Hayati Bernard Membe Mikocheni Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai, 2023.