Daily Archives: July 16, 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijjiria Zanzibar Tarehe 16 Julai, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Viongozi alipowasili katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Wanawake wa Kiislam na Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijiria tarehe 16 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wananchi mbalimbali kwenye Kongamano la Wanawake wa Kiislam katika Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijiria yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar tarehe 16 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Hati za Shukrani kwa baadhi ya Viongozi na Washiriki waliofanikisha kukamilika kwa Shughuli ya Kongamano la Wanawake wa Kiislam na Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijiria yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar tarehe 16 Julai, 2023.
.
.
.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa zawadi maalum iliyotolewa na Wanawake wa Kiislam kwenye Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijiria, yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar tarehe 16 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wanawake wa Kiislam mara baada ya kuzungumza nao kwenye Kongamano na Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijiria yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar tarehe 16 Julai, 2023.
Baadhi ya Viongozi na Wanawake wa Kiislam wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano na Maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kiislam 1445 Hijiria yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar tarehe 16 Julai, 2023.
.
.
.
.
.
.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AWAASA WANAWAKE KUSIMAMIA MAADILI YA JAMII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake kushikamana na kuilea jamii katika malezi yaliyo bora kimaadili ili kuiepusha jamii na vitendo viovu.

Rais Samia ametoa tamko hilo leo katika kongamano la wanawake wa Kiislam Zanzibar mwezi 27 katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu 1445 – Hijjiria lililofanyika ukumbi wa Golden Tulip.

Aidha, Rais Samia amesema kila mwanamke ana wajibu wa kusimamia maadili kwa kuwa ana mchango mkubwa sana katika kujenga au kumomonyoa maadili ya familia na jamii kwa ujumla.

Vile vile, Rais Samia amesema hivi sasa wanawake wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki na kushiriki katika masuala ya kitaifa na kijamii kwa kufanya kazi kwa uadilifu, uhakika na weledi mkubwa ambazo awali walidhaniwa hawaziwezi.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wanawake kujiepusha na vitendo vya unyanyasaji kwa kuwa vinarejesha nyuma maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Rais Samia pia amesema ukosefu wa elimu ya msingi ya dini unaathiri jamii na kusababisha vitendo vinavyokiuka maadili kama udhalilishwaji wa kijinsia, wizi na matumizi ya dawa za kulevya na kuliondoshea taifa heshima, haiba na kuua vizazi vyetu.

Hali kadhalika, Rais Samia amewasihi wanawake kujiendeleza kielimu na kujitokeza kutumia fursa za kimaisha kila zinapojitokeza ili waweze kuinusuru jamii kwa kupambana na changamoto zinazojitokeza.