Monthly Archives: August 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ahudhuria Mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Johannesburg nchini Afrika Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wakuu wa nchi na Serikali kwenye Mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa China Mhe. Xi Jinping kando ya Mkutano wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma hotuba yake kwenye Mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Senegal Mhe. Macky Sall kando ya mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa kando ya mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa pamoja na Rais wa Senegal Mhe. Macky Sall kando ya mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Malawi Mhe. Lazarus Chakwera kando ya mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Iran Mhe. Dkt. Seyyed Ebrahim Raisi kabla ya kuanza mazungumzo kando ya mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Iran Mhe. Dkt. Seyyed Ebrahim Raisi kando ya mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Viongozi Wakuu wa BRICS wakiwa kwenye Mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AHIMIZA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwahimiza waumini kujihusisha na shughuli za uzalishaji.

Rais Samia amesema hayo leo katika maadhimisho ya miaka 60 ya KKKT yaliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira.

Aidha, Rais Samia amesema dunia inakabiliwa na changamoto ya usalama wa chakula hivyo ni vyema nchi ikazalisha zaidi kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, ili tuendelee kujitosheleza kwa chakula na tuweze kulisha nchi za jirani na dunia kwa ujumla.

Wakati huo huo, Rais Samia amezitaka taasisi za dini kujiwekea mikakati mahsusi ya kupambana na uharibifu wa mazingira na utunzaji wa mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Vile vile, Rais Samia amesema mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kama ukame, mafuriko, kutotabirika kwa misimu na hivyo kuathiri kilimo kwa nchi yetu ambayo kwa asilimia kubwa tunategemea kilimo.

Rais Samia pia amesema Serikali imeelekeza jitihada kwenye kuwawezesha wananchi kutumia vyanzo mbadala vya nishati kama sehemu ya mkakati wa kuhifadhi mazingira.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.