Daily Archives: August 21, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AHIMIZA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwahimiza waumini kujihusisha na shughuli za uzalishaji.

Rais Samia amesema hayo leo katika maadhimisho ya miaka 60 ya KKKT yaliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira.

Aidha, Rais Samia amesema dunia inakabiliwa na changamoto ya usalama wa chakula hivyo ni vyema nchi ikazalisha zaidi kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, ili tuendelee kujitosheleza kwa chakula na tuweze kulisha nchi za jirani na dunia kwa ujumla.

Wakati huo huo, Rais Samia amezitaka taasisi za dini kujiwekea mikakati mahsusi ya kupambana na uharibifu wa mazingira na utunzaji wa mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Vile vile, Rais Samia amesema mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kama ukame, mafuriko, kutotabirika kwa misimu na hivyo kuathiri kilimo kwa nchi yetu ambayo kwa asilimia kubwa tunategemea kilimo.

Rais Samia pia amesema Serikali imeelekeza jitihada kwenye kuwawezesha wananchi kutumia vyanzo mbadala vya nishati kama sehemu ya mkakati wa kuhifadhi mazingira.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Mhe. Rais Samia amkabidhi Cheti Msanii na Muandaaji wa Filamu maarufu nchini China Jin Dong kama Balozi wa Utalii nchini tarehe 20 Agosti, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Muigizaji maarufu wa Filamu nchini China, Jin Dong cheti cha Ubalozi wa Heshima wa Kutangaza Utalii wa Tanzania nchini China wakati alipotembelea Jiji la Arusha tarehe 20 Agosti, 2023.
.
.
.