Monthly Archives: October 2023

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Tarehe 20 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe wakati alipomtembelea Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe wakati alipomtembelea Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Bendera (Pennant) ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kama kumbukumbu kutoka kwa Rais wa Shirikisho hilo Dkt. Patrice Motsepe Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshika zawadi yake ya Bendera (Pennant) ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kama kumbukumbu mara baada ya kupewa na Rais wa Shirikisho hilo Dkt. Patrice Motsepe Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro watatu kutoka (kulia), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma wa pili kutoka kulia, Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria Mhe. Jaji George Masaju wa kwanza (kulia), Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wa pili kutoka kushoto pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Neema Msitha wa kwanza (kushoto) mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Mboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023).

Maonesho haya yanatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kujifunza na kuwekeza katika kilimo hususan kwenye teknolojia rafiki ya mazingira.

Maonesho haya yanafanyika wakati dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na uhaba wa chakula.

Ili kupambana na hali hii uwekezaji wa mitaji kwenye sekta ya kilimo hasa sekta hiyo ndogo ya mboga na matunda imeonekana kuwa na umuhimu ili kuongeza usalama wa chakula duniani na kutunza mazingira kwa wakati mmoja.

Serikali ya Tanzania kupitia taasisi zake mbalimbali na sekta binafsi itashiriki katika maonesho haya kwa lengo la kutafuta masoko ya mazao ya kilimo.

Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikijitosheleza kwa chakula na sasa imeweka msukumo mkubwa kwenye uwekezaji wa kilimo hasa eneo la upatikanaji wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji, utafiti pamoja na upatikanaji wa mbolea nafuu na viuatilifu.

Juhudi hizi zinalenga kupunguza gharama za uzalishaji kwa mkulima na kuongeza tija na uzalishaji kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya ndani na ziada kuuza nchi nyingine.

Sekta ya mboga na matunda ni miongoni mwa sekta zinazokua kwa kasi kwa mwaka kati ya 7% hadi 11% na kutoa fursa za ajira kwa takriban watu milioni 6.5 hasa kwa vijana na wanawake.