Monthly Archives: October 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Bw. George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mandepo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usuluhishi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Bw. Mandepo anachukua nafasi ya Mhe. Griffin Venance Mwakapeje ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

  1. Amemteua Dkt. Saudin Jacob Mwakaje kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Dkt. Mwakaje ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza lililomaliza muda wake.
  1. Amemteua Bw. George Daniel Yambesi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kipindi cha pili.

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Oktoba, 2023.

Mhe. Rais Samia ashiriki Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) nchini Qatar Tarehe 02 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo cha Mbogamboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) nchini Qatartarehe 02 Oktoba, 2023.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ukumbini kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa  Kimataifa wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) nchini Qatar tarehe 02 Oktoba, 2023.
Shamrashamra za Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kilimo  cha Mbogamboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) nchini Qatar tarehe 02 Oktoba, 2023.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Amiri wa Taifa la Qatar Mhe. Sheikh Tamim Bin Hamad Al-Than wa pili kutoka kushoto kwake pamoja na viongozi wengine wakati wa Wimbo wa Taifa wa Qatar ukiimbwa kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa  Kimataifa wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) uliofanyika Doha tarehe 02 Oktoba, 2023.