Daily Archives: November 3, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezisihi nchi za Afrika kuandika upya kuhusu bara la Afrika kwa kuelezea simulizi zao wenyewe.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano nchini Rwanda.

Rais Samia amesema serikali za Afrika lazima zijitafakari upya ili utalii uweze kushamiri ikiwemo kujitangaza kimkakati, kufanya utafiti na uhifadhi.

Akisisitiza hilo, Rais Samia amesema katika zama hizi za taarifa potofu, Afrika haitakiwi kukaa kimya na badala yake ieleze ukweli wa bara hilo kwani muda ni sasa.

Aidha Rais Samia amesema iwapo kweli Afrika ikitaka kuendelea kuwa na vivutio vya asili ni lazima itoe kipaumbele kwenye uhifadhi na kuunga mkono jitihada za kutunza maeneo ya kiutamaduni, kazi za sanaa hususan za kihistoria na mila kwa vizazi vijavyo.

Utafiti, vivutio kwenye masuala ya utalii na athari za mazingira ni muhimu kwenye sekta hiyo ili umuhimu wake ubaki barani Afrika.

Wakati huo huo, Rais Samia amesisitiza wajibu wa sekta binafsi kwenye mfumo mzima wa utalii akihimiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano baina ya serikali, sekta binafsi pamoja na asasi zisizo za serikali.

Mhe. Rais Samia ashiriki Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC), Kigali nchini Rwanda Tarehe 02 Novemba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba,
2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakati wakielekea kwenye Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame pamoja na viongozi mbalimbali wakati wakishiriki Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Kikundi cha ngoma za Utamaduni chenye asili ya Rwanda kikitumbuiza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya Mkutano wa Kimataifa wa 23 wa Baraza la Utalii Dunian i(WTTC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kigali (Kigali Convention Centre) nchini Rwanda tarehe 02 Novemba, 2023.