Rais Samia Suluhu Hassan akabidhi nyumba kwa Mama Janeth Magufuli 05 Novemba, 2023 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla fupi ya kukabidhi nyumba ya kuishi iliyopo wilaya ya Kinondoni ambayo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufunguo mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli ikiwa ni ishara ya kukabidhi nyumba mpya ya kuishi kwa familia ya Dkt. John Pombe Magufuli iliyopo wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambayo amejengewa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa nyumba mpya ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, na kuikabidhi kwa Mama Janeth Magufuli, nyumba hiyo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan ampa pole Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alimpotembelea nyumbani kwake kumpa pole ya kufiwa na Kaka yake Issa Juma Ngalapa aliyefariki alfajiri ya leo, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023. .