Rais Samia Suluhu Hassan awapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Ikulu Tunguu Zanzibar Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Umri wa miaka 15 (CECAFA U-15) kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Mohamed Ali Mohamed wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Karume Boys, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Umri wa miaka 15 (CECAFA U-15) mara baada ya kukabidhiwa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Mohamed Ali Mohamed wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Karume Boys, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kipa Bora Gloves kutoka kwa Kipa bora wa Mashindano ya CECAFA U-15 Mahir Abdallah Amour wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Karume Boys, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.