Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Apokea Miradi Iliyofadhiliwa na Kujengwa na Serikali ya Ujerumani Kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG), katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Leo Tarehe 28 Julai, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata Utepe kwa ajili ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kulia ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bi. Regine Hess, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, kulia Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo, Waziri wa Afya Mhe. Doroth Gwajima, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa kwa ajili ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bi. Regine Hess.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo  kuhusu uchunguzi wa Magonjwa Ambukizi baada ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Chanjo ya Uviko 19 katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, Leo Tarehe 28 Julai, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Chanjo ya Uviko 19 katika Viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha Cheti cha Uthibitisho wa Chanjo muda mfupi baada ya kuzindua Chanjo ya Uviko 19.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipata Chanjo ya Uviko 19 ikiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria uzinduzi huo.