TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Visiwa vya Comoro kuratibu sekta binafsi pamoja na Serikali ili kutumia fursa za kibiashara zilizopo nchini humo kuhakikisha Tanzania inanufaika na mahitaji ya bidhaa mbalimbali katika nchi hiyo.

Mhe. Rais Samia amesema hayo tarehe 07 Novemba, 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma katika hafla ya kumuapisha Mhe. Pereira Ame Silima kuwa Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Visiwa vya Comoro.

Pia, Mhe. Rais Samia amesema mahitaji ya nchi ya Jamhuri ya Visiwa vya Comoro yanaitegemea Tanzania kwa zaidi ya asilimia 80 hivyo kutoa fursa kubwa ya biashara kwa Tanzania.

Aidha, Mhe. Rais Samia amemtaka Balozi Pereira kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya biashara, masuala ya kisiasa, na diplomasia kwa kuwa Tanzania na Comoro zina historia ya uhusiano wa muda mrefu.

Hafla ya kumuapisha Balozi Pereira imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Katanga, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Vincent Mbogo pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Serikali.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Afungua Kongamano la Kumbukizi ya Historia ya Maalim Seif Sharif Hamad Tarehe 05 Novemba, 2021 Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad lililofanyika tarehe 05 Novemba, 2021 katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Bi Awena Sinani Masoud aliyekua mke wa Hayati Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kufungua Kongamano la Kumbukizi ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad lililofanyika tarehe 05 Novemba, 2021 katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume walipokutana kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad lililofanyika tarehe 05 Novemba, 2021 katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Zanzibar kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad lililofanyika tarehe 05 Novemba, 2021 katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongozana na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Zanzibar kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad lililofanyika tarehe 05 Novemba, 2021 katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.