Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan azindua Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Misungwi mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuzindua mradi wa Maji utakaohudumia Mji wa Misungwi na maeneo ya pembezoni katika hafla iliyofanyika Misungwi mkoani Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada kuzindua mradi wa Maji utakaohudumia Mji wa Misungwi na maeneo ya pembezoni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa Maji utakaohudumia Mji wa Misungwi na maeneo ya pembezoni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia na kuyashika maji mara baada ya kuzindua mradi huo wa Maji utakaohudumia Mji wa Misungwi na maeneo ya pembezoni

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan afungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mwanza tarehe 13 Juni, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga kufungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza katika sherehe zilizofanyika Jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga, Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kufungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza katika sherehe zilizofanyika Jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyakazi wa Benki Kuu pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza katika sherehe zilizofanyika Jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Mwanza waliokuwa wakimsubiri nje ya Geti la Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza mara baada ya kumaliza hafla ya ufunguzi