Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Karatasi yenye majina ya viongozi mbalimbali walioshiriki kufanikisha kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR ) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341 mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR ) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1
Post navigation
← Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan atembelea na kukagua Daraja la JP Magufuli (Kigongo -Busisi) mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2021
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI →