MATUKIO MBALIMBALI YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI MWANZA KUANZIA TAREHE 13-15 JUNI, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Mkuyuni na Butimba Kona mara baada ya kusimama wakati akielekea kutembelea na kukagua Daraja la JP Magufuli mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Buhongwa mkoani Mwanza wakati akiendelea na ziara yake mkoani Mwanza
Wakina mama wa CCM Busisi wilayani Sengerema wakimpungia mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akiondoka eneo hilo mara baada ya kuwahutubia
Wananchi wa Mkuyuni na Butimba wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposimama eneo hilo kuwasalimu tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mama Mzazi wa (Mjane) Mama Janeth Magufuli, Mama Juliana Stephano Kidaso mara baada ya kuwasili Busisi Mkoani Mwanza katika muendelezo wa ziara yake tarehe 14 Juni, 2021

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *