Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipozuru Kaburi hilo tarehe Oktoba 14,2021. alipokua njiani akielekea katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kuzima Mwenye Maalum wa Uhuru. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride rasmi lililoandaliwa na Vijana wa Chipukizi Tanzania, alipowasili katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita .Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Kiongozi wa mbio za mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi kwa kutambua mchango wake mkubwa baada ya kuongoza kukimbiza Mwenge huo katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, wakati wa maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu......