Siku ya Pili ya Ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Oktoba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) alipowasili katika Hospitali ya KCMC Moshi kwa ajili  kuhudhuria sherehe ya Maadhimisho ya kumbukizi ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC leo tarehe 16 Oktoba, 2021 Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la Mionzi katika Hospitali ya KCMC Moshi wakati wa sherehe ya Maadhimisho ya kumbukizi ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC iliyofanyika leo tarehe 16 Oktoba 2021 Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mnara wa kumbukizi ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC iliyofanyika leo tarehe Oktoba 16,2021 Moshi Mkoani Kilimanjaro. Wa pili kulia Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Fredrick O. Shoo, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mollel, kushoto Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. na Katibu Mkuu wa CCM Cd Daniel Chongolo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa KKKT Dr. Fredrick O. Shoo, wa pili kulia, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mollel, kushoto Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. na Katibu Mkuu wa CCM Cd Daniel Chongolo, baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la Mionzi katika Hospitali ya KCMC Moshi wakati wa sherehe ya Maadhimisho ya kumbukizi ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC iliyofanyika leo tarehe 16 Oktoba 2021 Moshi Mkoani Kilimanjaro.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu Mnara wa Kumbukizi ya Maadhimisho ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 16 Oktoba 2021, baada ya kuzindua Mnara huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua kitabu cha mpango wa utekelezaji wa Maadhimisho ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Oktoba 2021. Kulia ni  Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt.  Fredrick O. Shoo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt.  Fredrick O. Shoo baada ya kuhutubia kwenye Sherehe ya Kumbukizi ya Maadhimisho ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Sherehe ya Kumbukizi ya Maadhimisho ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Oktoba 2021.
.
Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt.  Fredrick O. Shoo akimkabidhi Tuzu ya Maadhimisho ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua Juhudi zake kwa Taifa, tarehe 16 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kikatiti alipokua njiani akitokea Mkoani Kilimanjaro akielekea Mkoani Arusha kuendelea na ziara yake ya kikazi tarehe 16 OKtoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Usariva alipokua njiani akitokea Mkoani Kilimanjaro akielekea Mkoani Arusha kuendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha tarehe 16 OKtoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Tengeru alipokua njiani akitokea Mkoani Kilimanjaro akielekea Mkoani Arusha kuendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha tarehe 16 OKtoba, 2021.
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *