Mapokezi ya Mhe. Rais Uhuru Kenyatta , Ikulu Jijini Dar es Salaam Leo tarehe 10 Desemba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 202. Mhe. Rais Uhuru Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakipokea wimbo wa Mataifa mawili Tanzania na Kenya wakati Mhe. Rais Kenyatta alipowasili katika viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021. Mhe. Rais Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.
Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akikagua gwaride rasmi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania apowasili katika viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021, Rais Uhuru Kenyatta yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali ya siku moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakiwa katika picha yenye waasisi wa Mataifa mawili Tanzania na Kenya Hayati Mwalim Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Jomo Kenyatta wa Kenya wakati Rais Kenyatta alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021. Mhe. Rais Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati Rais Kenyatta alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021. Mhe. Rais Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *