Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 17 Desemba, 2021 amezungumza kwa njia ya simu na Wakuu wa Shule za Sekondari wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi unaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Samia amewaeleza walimu hao kuwa kutokana na majukumu mengi ya kikazi ameshindwa kuhudhuria Mkutano huo lakini anaufatilia kwa karibu na yupo pamoja nao.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema anatambua masuala yao mbalimbali ambayo Serikali inayafanyia kazi na hivyo kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidi ili kutimiza wajibu wao.
Pia, Mhe. Rais Samia amewapongeza na kuwatakia heri katika Mkutano huo Mkuu wa Walimu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi unaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa 16 unawaleta pamoja Wakuu wa Shule ili kubadilishana mawazo, uzoefu, changamoto, mafanikio na utekelezaji wa Sera na mipango inayotolewa na Serikali na unahudhuriwa na walimu 5,156 kutoka shule za Sekondari za Serikali na Shule za Sekondari binafsi.