Mhe. Rais Samia Azindua Tamasha la Kwanza la Utamaduni la mkoa wa Kilimanjaro Leo Tarehe 22 Januari, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Chakula cha asili na zana mbalimbali za asili ya Kabila la Kichaga kutoka kwa Chifu Prosper wa Kabila hilo, wakati alipotembelea maonesho katika Uzinduzi wa Tamasha la kwanza la Utamaduni wa Mkoa wa Kilimanjaro lililozinduliwa leo tarehe 22 Januari 2022 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Chakula cha asili na zana mbalimbali za asili ya Kabila la Kimasai kutoka kwa Chifu Jeremia Laizer, wakati alipotembelea maonesho katika Uzinduzi wa Tamasha la kwanza la Utamaduni wa Mkoa wa Kilimanjaro lililozinduliwa leo tarehe 22 Januari, 2022 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi.
.
Chief Mkuu wa Kabila la Kichaga Chief Mareale akimkabidhi Ngao na Mshale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kama ishara ya kumkaribisha rasmi kwenye kabila hilo wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la kwanza la Utamaduni wa Mkoa wa Kilimanjaro lililozinduliwa tarehe 22 Januari, 2022 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwapungia mkono Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwahutubia katika Uzinduzi wa Tamasha la kwanza la Utamaduni wa Mkoa wa Kilimanjaro katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi tarehe 22 Januari, 2022.
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *