Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Aondoka Nchini Kwenda Nchini Ufaransa kwa Ziara ya Kikazi Tarehe 09 Februari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Husein Ali Mwinyi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea Nchini Ufaransa tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wazee wa Zanzibar waliofika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume  kabla ya kuondoka na kuelekea nchini Ufaransa  tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili Paris nchini Ufaransa kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu rasilimali bahari Duniani tarehe 10 Februari, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *