Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ahutubia katika Siku ya Kitaifa ya Tanzania katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 Tarehe 26 Februari, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, pamoja na wananchi kutoka Mataifa mbalimbali Duniani katika Siku ya Kitaifa ya Tanzania katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 yanayofanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Ustahimilivu na Uhusiano ambaye pia ni Kamishna wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 Sheikh Nahayan Mabarak Al Nahayan wakati akielekea katika Banda la Maonesho la Tanzania lililopo Dubai
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuonesha picha ya vito mbalimbali vilivyotengenezwa kwa Madini ya Tanazanite ambayo yanapatikana Tanzania pekee wakati walipofika katika banda la maonesho la Tanzania katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 yanayofanyika Dubai, UAE.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Ustahimilivu na Uhusiano ambaye pia ni Kamishna wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 Sheikh Nahayan Mabarak Al Nahayan mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania pamoja na la Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika maonesho hayo ya Dubai Expo 2020.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda mbalimbali ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika maonesho hayo ya Dubai Expo 2020 leo tarehe 26 Februari, 2022.
.
.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha kumbukumbu mara baada ya mazungumzo na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE na Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *