TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA APOKEA KOMBE LA DUNIA (WORLD CUP) JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepokea Kombe la Dunia (World Cup) litakaloshindaniwa kwenye mashindano ya Mpira wa Miguu nchini Qatar kuanzia 21/11 – 18/12/2022.

Rais Samia amepokea Kombe hilo kutoka kwa Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambaye ni mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil Juliano Belletti katika hafla iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Pia Rais Samia amesema ujio wa Kombe la Dunia Tanzania utaleta fursa za kiuchumi hivyo kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kwa manufaa ya taifa.

Aidha, Rais Samia amewataka Watanzania kutumia fursa zinazojitokeza kuitangaza na kuisemea vizuri Tanzania na kuzitumia fursa hizo kibiashara kwa kuuza bidhaa halisi za kitanzania vikiwemo vyakula.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali imeanzisha Mfuko wa Kukuza Vipaji, hivyo kuwataka viongozi kuzitumia vizuri fedha zinazotolewa kwa madhumuni hayo na kuwaandaa vijana kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali, baadhi ya wachezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ akiwemoSunday Manara na Abdallah Kibadeni pamoja na wadau wengine wa michezo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *