TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA). Meja Jenerali Semfuko anaendelea na kipindi cha pili baada ya kumaliza kipindi cha kwanza.
  1. Amemteua Prof. Sebastian Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI). Prof. Chenyambuga ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *