TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

  1. Amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.
  1. Amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.
  1. Amempangia kituo Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
  1. Amemteua Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi. Dkt. Suleiman ni Afisa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Julai, 2022 na uapisho utafanyika leo tarehe 20 Julai, 2022 saa 05:00 Asubuhi Ikulu, Chamwino Dodoma.

Wakati huo huo, Mhe. Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: –

  1. Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki. Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.
  1. Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.
  1. Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;
  1. Amempandisha Cheo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi Jamii. Anachukua nafasi ya CP Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu mengine.
  • Amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *