TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA).

Dkt. Sweke anachukua nafasi ya Bw. Zahor Kassim El-Kharousy ambaye amemaliza kipindi chake.

Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Sweke alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Julai, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *