TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MBEYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha huduma ya maji safi kwa wananchi katika miradi inayozinduliwa inakuwa endelevu.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua Mradi wa Maji wa Shongo – Mbalizi mkoani Mbeya uliogharimu shilingi bilioni 3.345.

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi inawafikia wananchi kwa uhakika kwa kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa jengo la afya ya huduma ya mama na mtoto hospitali ya Meta ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia akina mama zaidi ya 300 litakapokamilika.

Ujenzi wa jengo hilo utakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kina mama wa mkoa huo na kutoka mikoa mingine ya Nyanda za juu Kusini.

Vile vile Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kuwataka madiwani mkoani humo kuhakikisha kuwa asilimia 10 ya Halmashauri inatumika katika miradi ya maendeleo.

Rais Samia yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *