TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI CHUNYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI kupitia Halmashauri zote nchini na kuhakikisha zinaweka mipango ya kukusanya mapato.

Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Chunya -Makongolosi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 39 iliyofanyika katika uwanja wa Matundasi.

Aidha, Rais Samia amesema mapato yanayokusanywa na Halmashauri yakisimamiwa vizuri yanaweza kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Chunya mjini, Rais Samia ameagiza Madiwani na Wenyeviti wa eneo hilo wanaopata mapato mengi kutokana na kutoa leseni nyingi za biashara kujenga kituo cha mabasi cha Chunya.

Vile vile, Rais Samia ameeleza barabara hiyo itafungua fursa za kibiashara kwa wananchi wa Chunya kwani inaunganisha mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *